Mhubiri 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mhubiri 5 (Swahili) Ecclesiastes 5 (English)

Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya. Mhubiri 5:1

Guard your steps when you go to God's house; for to draw near to listen is better than to give the sacrifice of fools, for they don't know that they do evil.

Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu; kwa maana, Mungu yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache. Mhubiri 5:2

Don't be rash with your mouth, and don't let your heart be hasty to utter anything before God; for God is in heaven, and you on earth. Therefore let your words be few.

Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno. Mhubiri 5:3

For as a dream comes with a multitude of cares, so a fool's speech with a multitude of words.

Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri. Mhubiri 5:4

When you vow a vow to God, don't defer to pay it; for he has no pleasure in fools. Pay that which you vow.

Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe. Mhubiri 5:5

It is better that you should not vow, than that you should vow and not pay.

Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba umepitiliwa; kwani Mungu akukasirikie sauti yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako? Mhubiri 5:6

Don't allow your mouth to lead you into sin. Don't protest before the messenger that this was a mistake. Why should God be angry at your voice, and destroy the work of your hands?

Maana ndivyo ilivyo katika habari za wingi wa ndoto, na ubatili, na maneno mengi; walakini wewe umche Mungu. Mhubiri 5:7

For in the multitude of dreams there are vanities, as well as in many words: but you must fear God.

Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao. Mhubiri 5:8

If you see the oppression of the poor, and the violent taking away of justice and righteousness in a district, don't marvel at the matter: for one official is eyed by a higher one; and there are officials over them.

Lakini, pamoja na hayo, manufaa ya nchi kwa kila njia ni mfalme anayejibidiisha kwa ajili ya shamba. Mhubiri 5:9

Moreover the profit of the earth is for all. The king profits from the field.

Apendaye fedha hatashiba fedha, Wala apendaye wingi hatashiba maongeo. Hayo pia ni ubatili. Mhubiri 5:10

He who loves silver shall not be satisfied with silver; nor he who loves abundance, with increase: this also is vanity.

Mali yakiongezeka, hao walao nao waongezeka na mwenyewe hufaidiwa nini, ila kuyatazama kwa macho yake tu? Mhubiri 5:11

When goods increase, those who eat them are increased; and what advantage is there to its owner, except to feast on them with his eyes?

Usingizi wake kibarua ni mtamu, kwamba amekula kidogo, au kwamba amekula kingi; lakini kushiba kwake tajiri hakumwachi kulala usingizi. Mhubiri 5:12

The sleep of a laboring man is sweet, whether he eats little or much; but the abundance of the rich will not allow him to sleep.

Kuna na balaa mbaya sana niliyoiona chini ya jua, nayo ni hii, mali alizoziweka mwenyewe kwa kujinyima; Mhubiri 5:13

There is a grievous evil which I have seen under the sun: wealth kept by its owner to his harm.

na mali hizo zimepotea kwa bahati mbaya; naye akiwa amezaa mwana, hamna kitu mkononi mwake. Mhubiri 5:14

Those riches perish by misfortune, and if he has fathered a son, there is nothing in his hand.

Alivyotoka tumboni mwa mamaye, atakwenda tena tupu-tupu kama alivyokuja; asichume kitu cho chote kwa ajili ya kazi yake, hata akichukue mkononi mwake. Mhubiri 5:15

As he came forth from his mother's womb, naked shall he go again as he came, and shall take nothing for his labor, which he may carry away in his hand.

Hiyo ndiyo balaa mbaya sana, ya kwamba kama vile alivyokuja, vivyo hivyo atakwenda zake; naye amefaidiwa nini mwenye kujitaabisha kwa ajili ya upepo? Mhubiri 5:16

This also is a grievous evil, that in all points as he came, so shall he go. And what profit does he have who labors for the wind?

Siku zake zote hula gizani, mwenye fadhaa nyingi, mwenye ugonjwa na uchungu. Mhubiri 5:17

All his days he also eats in darkness, he is frustrated, and has sickness and wrath.

Tazama, mimi niliyoyaona kuwa ndiyo mema na ya kufaa, ni mtu kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote anayoifanya chini ya jua, siku zote za maisha yake alizopewa na Mungu; maana hilo ndilo fungu lake. Mhubiri 5:18

Behold, that which I have seen to be good and proper is for one to eat and to drink, and to enjoy good in all his labor, in which he labors under the sun, all the days of his life which God has given him; for this is his portion.

Tena, kwa habari za kila mwanadamu, ambaye Mungu amempa mali na ukwasi, akamwezesha kula katika hizo, na kuipokea sehemu yake, na kuifurahia amali yake; hiyo ndiyo karama ya Mungu. Mhubiri 5:19

Every man also to whom God has given riches and wealth, and has given him power to eat of it, and to take his portion, and to rejoice in his labor--this is the gift of God.

Kwa kuwa mtu hatazikumbuka mno siku za maisha yake; kwa sababu Mungu humtakabali katika furaha ya moyo wake. Mhubiri 5:20

For he shall not often reflect on the days of his life; because God occupies him with the joy of his heart.